Advertisement

Bongo Flava Atimiza Miaka 30: Sherehe Kubwa Mlimani City Leo na Diamond na Alikiba Na Wakongwe Wangine Kwenye Jukwaa moja la Burudaniii.

Bongo Flava Atimiza Miaka 30: Sherehe Kubwa Mlimani City Leo na Diamond na Alikiba Na Wakongwe Wangine Kwenye Jukwaa moja la Burudaniii.

Mwanza / Dar es Salaam. Hatimaye siku ambayo mashabiki wengi wa muziki wa Tanzania wamekuwa wakiisubiri imewadia. Leo jumatatu ya Septemba 28, 2026, ukumbi wa Mlimani City Hall unahost sherehe kubwa ya kuhitimisha maadhimisho ya Miaka 30 ya Bongo Flava.

Sherehe hizi zinafanyika siku chache tu baada ya tamasha la Arusha lililofanyika Septemba 19 kwenye viwanja vya General Tyre. Kama unakumbuka, tamasha hilo liliibua mjadala baada ya Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kuchukua hatua dhidi ya msanii Dudu Baya. Leo Dar es Salaam ndio pazia linafungwa kwa kishindo.

Wasanii Gani Wapo Ndani ya Mlimani City Sasa Hivi?

Taarifa kutoka kwa waandaaji wa Bongo Flava Honors inaeleza kuwa zaidi ya wasanii 50 wamealikwa. Hadi sasa waliopo ndani ni:

Diamond Platnumz kutoka WCB Wasafi, Alikiba kutoka Kings Music, Harmonize wa Konde Gang, pamoja na Marioo, Zuchu, Nandy, Rayvanny, Jux, Mbosso na TID. Wasanii wakongwe kama Dully Sykes na Professor Jay pia wameonekana eneo la tamasha.

Kitendo cha Diamond na Alikiba kuonekana eneo moja ndicho kinachosubiriwa zaidi na mashabiki, kwani kwa muda mrefu hawajashiriki jukwaa moja pamoja.

Kwa Nini Miaka 30 ya Bongo Flava ni Muhimu?

Muziki wa Bongo Flava ulianza kupata sura yake miaka ya 1990 kupitia makundi ya Hard Blasters na wasanii kama Saleh Jabir. Kutoka kwenye kanda za kaseti mpaka leo kufika kwenye majukwaa ya kimataifa na chati za Billboard, safari imekuwa ndefu. Ndio maana BASATA na wadau wengine wameamua kutoa heshima hii.

Lengo la waandaaji sio tu burudani, bali ni kutoa maua kwa waasisi wa muziki huu wakiwa hai na kuwaenzi kwa mchango wao.

Ratiba ya Tamasha la Leo Mlimani

Kwa mujibu wa timu yetu iliyopo Dar, milango ilifunguliwa mapema saa nne asubuhi. Mpaka sasa mchana, mashabiki zaidi ya elfu tano wameingia ndani. DJ Joozey anaendelea kupiga mchanganyiko wa nyimbo kali za zamani kama Nikusaidiaje na Mpenzi.

Wasanii wakubwa wanatarajiwa kuanza kutumbuiza kuanzia saa moja usiku na tamasha linatarajiwa kumalizika saa sita usiku. Kiingilio ni bure kwa yeyote aliye ndani ya Mlimani City. Kama upo Mwanza kama sisi, unaweza kufuatilia moja kwa moja kupitia YouTube ya Wasafi TV na Clouds TV.

Team ya Edutipers ipo Mlimani, tutakuletea video na picha kila baada ya dakika chache. Endelea kutufuatilia.

More from Edutipers.com

1,TOXIC - MIMI LINI [Official Audio] 2026 | Download Mp3, 

2,Lomodo - Fire Burn Mp3 Download

3,Toneb Ft Lody Music - Roho Mp3 Download 2026 .

Upo wapi unafatilia tamasha? Andika kwenye comment hapa chini.

Post a Comment

0 Comments